Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa FAO asisitiza uhusiano kati ya maendeleo vijijini na uhamiaji

Kilimo vijijini.(Picha ya FAO)

Mkurugenzi wa FAO asisitiza uhusiano kati ya maendeleo vijijini na uhamiaji

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula na Kilimo, José Graziano da Silva amesema kama nchi za Mediterenia zinataka kuzuia wimbi la uhamiaji na mateso ya binadamu basi ni lazima zijielekeze  katika kilimo, chakula na maendeleo ya vijijini kama msingi wa ushirikiano wa kikanda.Bw da Silva amesema haya leo wakati wa mkutano wa mataifa ya Ulaya na Mediternia kuhusu kilimo uliofanyika Palermo, Italia na kusisitiza uhusiano kati ya kilimo na uhamiaji, na umuhimu wa kuwekeza katika maendelo vijijini hususani kwa vijana.

Mathalan, da Silva amesema njia mabadala ya kuongeza motisha kwa vijana kushiriki katika shughuli ya vijijini, kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi na ufugaji wa samaki katika jamii na nchi zao.

Halikadhalika, amesema kuongeza kilimo ujasiriamali na fursa za ajira kwa vijana vijijini inahitaji kuwa msingi wa mikakati ya kupambana na umaskini na kukuza  maendeleo.