Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili wa kijinsia waangaziwa Uganda na Burundi

Kataa ukatili dhidi ya wanawake na peleka matumaini. (Picha:UN-Women)

Ukatili wa kijinsia waangaziwa Uganda na Burundi

Ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wa kike umeendelea kushamiri maeneo mbali mbali duniani ukisababisha makundi hayo kushindwa kushamiri kisiasa, kijamii na kiuchumi. Na hali inakuwa mbaya zaidi pindi kitendo hicho kinapofanywa na mtu ambaye anaaminika zaidi na makundi hayo, awe ni ndugu wa kijamii au mtu alipatiwa dhamana ya kuwasimamia ulinzi wao. Umoja wa Mataifa unataka matumaini yapelekwe kwa makundi hayo ili yaweze kustawi. Jarida hili maalum limemulika hali ilivyo huko Uganda na baadaye Burundi.