Vikwazo , ukiritimba katika biashara vikiondolewa vitakuza biashara : Mero

26 Novemba 2014

Mkutano kuhusu uwuishaji wa biashara ikiwamo kuondoa vikwazo na ukiritimba katika usafirishaji wa bidhaa zinazovuka mipaka umefanyika mjini Geneva Uswis ukiratibiwa na shirika la biashara duniani WTO.

Mkutano huu ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya makataba wa Bali unaotaka uboreshwaji wa biashara, kuruhusu nchi zinazoendelea kuwa na fursa zaidi katika kuimarisha  usalama wa chakula pamoja na kuinua biashara na maendeleo ya  nchi maskini.

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Modest Mero ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo.

(SAUTI MERO)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud