Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinga ya wafanyakazi dhidi ya mionzi ya nyuklia kumulikwa kwenye kongamano la IAEA

Wafanyakazi kwenye mtambo wa Fukushima. Picha@IAEA

Kinga ya wafanyakazi dhidi ya mionzi ya nyuklia kumulikwa kwenye kongamano la IAEA

Kongamano la kimataifa kuhusu jinsi ya kuwalinda watu ambao kazi zao zinawaweka hatarini kuathiriwa na mionzi ya nyuklia litafanyika kwenye makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, mjini Vienna, Austria kuanzia tarehe 1 hadi 5 Disemba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na IAEA, sekta ambako wafanyakazi wanakuwa kwenye mazingira ya miyonzi ya nyuklia ni kama vile ya afya, na ya ujenzi na ubomoaji wa mitambo ya nishati ya nguvu za nyuklia.

Jambo la kumulikwa zaidi litakuwa kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya wahudumu wa afya ambao wanaathiriwa na mazingira yenye mionzi ya nyuklia. Mada nyingine ya kuangaziwa ni ulinzi wa wafanyakazi katika hali za dharura kama ajali ya mtambo wa Fukushima Daiichi.