Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lapitisha maazimio sita kuhusu Palestina

Picha ya UM/Maktaba

Baraza Kuu lapitisha maazimio sita kuhusu Palestina

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha maazimio sita kuhusu Palestina, kufuatia ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali Mashariki ya Kati.

Maazimio hayo ni pamoja na azimio nambari 69/20 linalohusiana na kuwekwa kwa Kamati inayohusika na kufurahia kwa haki za msingi za watu wa Palestina likipata, azimio nambari 60/22 kuhusu kuwekwa idara inayohusika na haki za Palestina kwenye Sekritariati ya Umoja wa Mataifa, na azimio nambari 69/22 kuhusu programu ya habari kuhusu suala la Palestina kwenye Sekritariati ya Umoja wa Mataifa.

Maazimio mengine ni nambari 69/23 linalohusu suluhu la amani kwa suala la Palestina, azimio nambari 69/24 linalohusu mji wa Jerusalem na azimio nambari 69/25 kuhusu milima ya Golan. Maazimio matatu yamepata wingi kura zaidi ya 140, na matatu yakipata uungwaji mkono kwa kati ya kura 90 na 100 pekee. Maazimio yote yalipingwa na Israel, Marekani, Canada, Palau, Micronesia, Visiwa vya Marshall, na Australia ambayo ilipinga matatu, na kutoonyesha msimamo wake kwa matatu mengine.

Kutoka Afrika Mashariki, Tanzania pekee ndiyo iliyounga mkono maazimio yote, lakini Kenya, Burundi, Rwanda na Uganda hazikuonyesha misimamo kabisa.