Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna atiwa hofu na kiwango kisichowiana cha wamarekani weusi wanaouawa

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephen Dujarric.(Picha UM/Maktaba)

Kamishna atiwa hofu na kiwango kisichowiana cha wamarekani weusi wanaouawa

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ameelezea wasiwasi wake juu ya idadi ya isiyowiana ya vijana wamarekani weusi wanaofariki dunia wakati wa makabiliano na polisi.

Kamishna Zeid amesema hayo kufuatia jopo la waamuzi wa mahakama huko Ferguson, jimbo la Missouri nchini Marekani kutangaza kutokuona uthibitisho wowote wa kuweza kumfungulia mashtaka afisa polisi anayedaiwa kumuua Michael Brown, mmarekani mweusi mwezi Agosti mwaka huu.

Hata hivyo pamoja na kutuma rambirambi kwa familia ya kijana huyo, amesihi wakazi wa eneo hilo kujizuia na ghasia huku akielezea wasiwasi wake kama alivyozungumza Stephen Dujarric ni msemaji wa Umoja wa Mataifa.

(Sauti ya Dujarric)

Kamishna Mkuu anasema kwa wakati huu, hawezi kueleza iwapo uamuzi uliotolewa unakidhi sheria ya haki za binadamu ya kimataifa. Hata hivyoo anasema anatiwa hofu na kiwango kisichowiana cha idadi ya vijana wamarekani weusi wanaokufa katika makabiliano na polisi, halikadhalika idadi isiyowiana ya kundi hilo walioko magerezani au wanaosubiri adhabu ya  kifo.”

Halikadhalika ametoa wito kwa mamlaka..

(Sauti ya Dujarric)

"Kamishna Mkuu amesihi mamlaka za Marekani kufanya uchunguzi wa kina jinsi masuala ya rangi yanavyoathiri usimamizi wa haki na sheria, katika ngazi ya majimbo na serikali kuu.”