Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nusu ya visa vipya vya saratani 2012 vilitokana na utipwatipwa:Utafiti

Nembo ya WHO

Nusu ya visa vipya vya saratani 2012 vilitokana na utipwatipwa:Utafiti

Shirika la afya duniani , WHO kupitia taasisi yake inayohusika na tafiti za saratani, IARC imesema nusu ya visa vipya vya saratani mwaka 2012 vilisababishwa na utipwatipwa.

IARC ilifanya utafiti huo uliochapishwa leo kwenye jarida la Lancet ukionyesha kuwa watu hao Laki Nne na Elfu Themanini na Mmoja ni sawa na asilimia 3.6 ya wagonjwa wote wapya ikisema kuwa unene kupita kiasi na utipwatipwa uko zaidi nchi zilizoendelea kuliko zile zinazoendelea.

Matokeo hayo  yalizingatia kiwango cha uwiano kati ya uzito na urefu wa mtu, Body Mass Index ambapo katika takwimu hizo eneo la Amerika ya Kaskazini ndio lililoathiriwa zaidi, kwa kuwa na visa zaidi ya Laki Moja.

Mkurugenzi wa IARC , Christopher Wild amesema idadi ya wagonjwa wa saratani wanaohusishwa na unene kupindukia na utipwatipwa inatarajiwa kuongezeka kimataifa sambamba na maendeleo ya kiuchumi