Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tubadili mtazamo dhidi ya madhila yanayokumba wanawake:Ban

UN Photo/Eskender Debebe
Picha:

Tubadili mtazamo dhidi ya madhila yanayokumba wanawake:Ban

Katika maadhimisho ya siku hiyo ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema sasa ni wakati wa kuchukua hatua akizingatia maudhui ambayo ni peleka matumaini kwenye eneo lako la jirani kama njia ya kutokomeza ukatili huo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace) 

Tukio maalum kwa siku hii limefanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo ukumbi ulisheheni rangi ya Chungwa, ambayo ni rangi iliyochaguliwa na Umoja wa Mataifa kuashiria matumaini.

Hata Katibu Mkuu Ban Ki-moon alionyesha mshikamano kwa kuvalia tai ya rangi ya chungwa huku akifananisha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kama gonjwa lililolipuka duniani kote likiharibu maisha, mifumo ya jamii na hata kukwamisha maendeleo kuanzia Asia, hadi Afrika, Amerika hadi Ulaya.

Amesema ukatili hufanyika wakati Amani, na wakati wa mizozo hali huwa mbaya zaidi hivyo...

“Ni kwa kubadili uzoefu wa kila siku unaopata wanawake na wasichana ndio tutaweza kutokomeza ubagzi na ukwepaji sheria na kumaliza vitendo na mila zinazopuuzia au kuvumilia ghasia dhidi yao.”