Tumevuka lengo la tiba na mazishi, juhudi zinahitajika : Banbury
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola UNMEER Athony Bunbury amesema ujumbe huo umevuka malengo yake ya kutoa tiba kwa asilimia 70 ya wagonjwa na kuzika asilimia hiyo hiyo kwa njia salama.
Katika mahojiano na gazeti la Newsweek la Marekani Bwana Banbury amesema lengo hilo ambalo linapaswa kufikiwa ifikapo Disemba mosi mwaka huu limevuka kwa baadhi ya maeneo lakini akaonya kuwa huenda lisitimizwe katika baadhi ya maeneo.
Mkuu huyo wa UNMEER amesema maeneo ya vijijini nchini Sierra Leone, eneo liitwalo Makeni na Port Loko ni ya kutiiwa mkazo zaidi na kuomgeza kuwa juhudi za jumuiya ya kimataifa zinahitajika.