Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko kwa uchaguzi wa kidemokrasia; Ban aieleza Tunisia

UN Photo/Eskinder Debebe)
Fundi urembo nchini Tunisia akiwa katika moja ya shughuli zake. (Picha:

Heko kwa uchaguzi wa kidemokrasia; Ban aieleza Tunisia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewatumia salamu za heko wananchi wa Tunisia kwa kushiriki kwa amani uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo tangu mapinduzi ya mwaka 2011.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Ban akisema kuwa upigaji kura ulioendeshwa kwa kanuni na amani ni hatua muhimu katika mchakato wa mpito wa kisiasa nchini Tunisia.

Katibu Mkuu amesifu mamlaka huru ya ngazi ya juu ya uchaguzi kwa kazi waliyofanya na jitihada zao zinazoendelea za kukamilisha mchakato huo akisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia harakati za demokrasia nchini humo.