Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa WHO azuru Mali kupigia chepuo juhudi za UM kudhibiti Ebola

Mkurugenzi wa WHO azuru Mali kupigia chepuo juhudi za UM kudhibiti Ebola

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Dr Margaret Chan, amekutana na Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta, Waziri Mkuu Moussa Mara, na viongozi wengine wa serikali ili kujadili jitihada zinazoendelea za kukabiliana na mlipuko wa kirusi cha Ebola nchini humo, na jinsi mashirika ya Umoja Mataifa yataweza kuongeza misaada yao.

Dkt. Chan amezuru Mali wakati serikali ya nchi hiyo ikiwa imetangaza kisa kipya cha Ebola huku wagonjwa wengine wawaili wanaohofiwa kuambukizwa Ebola wakichunguzwa.

Akipongeza juhudi za serikali ya Mali za kupambana na Ebola, Dkt. Chan amesema, katika kipindi cha wiki kadhaa, Mali imewatambua kwa haraka watu ambao wamegusana na watu walioambukizwa Ebola, na juhudi hizi, Chang ameongeza ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Aidha, Bi Chan amesema ni muhimu kwa WHO na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Mali kusaidia serikali hadi mlipuko wa Ebola utakapodhibitiwa