Shambulizi la kigaidi Kenya, Ban alaani, atuma rambirambi

23 Novemba 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani shambulio la kigaidi dhidi ya basi la abiria huko Mandera nchini Kenya ambako watu wapatao 28 waliuawa.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Ban akituma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo la Jumamosi asubuhi huku akieleza mshikamano na wananchi na serikali ya Kenya.

Katibu Mkuu ameahidi ushirikiano wa Umoja wa Mataifa kwa serikali ya Kenya na nchi jirani katika jitihada za pamoja za kushughulikia ugaidi.

Halikadhalika Ban amesema ni matumaini yake kuwa wahusika wa shambulio hilo la leo watafikishwa haraka mbele ya sheria.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter