Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani irejee Sudan Kusini ili maisha yaendelee: Kang Kyung-Wha

Amani irejee Sudan Kusini ili maisha yaendelee: Kang Kyung-Wha

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu misaada ya kibinadamu Kang Kyung-Wha amesema ni lazima amani irejee Sudani Kusini ili watu warejee nyumbani na kujenga maisha upya.

Akizungumza na waaandishi wa habari baada ya ziara yake ya siku tatu nchini humo kiongozi huyo ambaye alitembelaa Sudan Kusini mwaka jana amesema hali ya kibinadamu ni tete kwani watu wanalazimishwa kukimbia makwao kutokana na mapigano akilinganisha alichoshuhudia mwaka jana na mwaka huu.

(SAUTI KANG KYUNG-WHA)

“Ukienda mbugani kule nje, kwa mfano pale tulipokuwa jana, utaona watu waliolazimishwa na mzozo kuhama, na sasa hawana chochote. Na idadi hii sasa ni karibu milioni 1.4 ndani ya nchi na takriban nusu milioni ni wakimbizi katika nchi jirani. Kwa hiyo, huo ndio mzigo wa kibinadamu tunaokabiliwa nao.”