Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 10,000 wapoteza makazi CAR:OCHA

UN photo / Catianne Tijerina
Mkimbizi wa ndani akiwa amerejea kwenye makazi yake mchana ili kutekeleza shughuli zake na jioni hurejea kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani. (Picha:

Zaidi ya watu 10,000 wapoteza makazi CAR:OCHA

Mapigano mapya kwenye kitongoji cha Zémio kusini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika  ya Kati, CAR yamesababisha majeruhi wapatao 10 na watu zaidi ya Elfu Kumi kukimbia makazi yao.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema mapigano hayo mapya baina ya jamii kwenye kitongoji hicho kilicho mpakani na Sudani Kusini yaliibuka kati ya tarehe 17 na 18 mwezi huu.

OCHA inasema asilimia 80 ya wakazi 16,000 wa kitongoji hicho sasa wanasaka hifadhi baada ya mashambulio hayo.

Jens Learke ni msemaji wa OCHA mjini Geneva.

(Sauti ya Jens)

“Hali katika mji wa Zémio ni ya wasiwasi mkubwa, Kuna watu wenye silaha, bunduki, mapanga, visu, pinde na mishale mjini humo, na tumepata taarifa hizi sasa hivi, na zimekuja kwa mshangao mkubwa, hata kwa wale wanaofanya kazi eneo hilo.”