Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji ya polisi wa Umoja wa Mataifa yameongezeka maradufu: Ladsous

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

Mahitaji ya polisi wa Umoja wa Mataifa yameongezeka maradufu: Ladsous

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous amesema kipindi cha miaka Kumi na Mitano kimeshuhudia kuongezeka kwa kiwango, upeo na umuhimu wa Polisi wa Umoja wa Mataifa.

Akihutubia Baraza la Usalama hivi leo, Bw Ladsous amesema ongezeko hilo linatokana na changamoto wanazokumbana nazo wakiwa maeneo ya kazi na hivyo kulazimu kubadili mwelekeo wa utendaji.

(SAUTI LADSOUS )

“Kushughulikia matatizo ya kawaida dhidi ya ugaidi, uhalifu wa kupangwa, ufisaji, naamini hii ni hali halisi inayokumba maafisa polisi wetu, na ningalipenda kutoa shukrani kubwa kwa ujasiri wao na firka zao walizodhihirisha pindi wanapokumbwa na mazingira magumu.”

Mwingine aliyehutubia Baraza la Usalama ni, Kamishna wa Polisi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, Greg Hinds ambaye alisema ili kuwepo kwa ufanisi katika ujenzi wa taasisi za nchi husika, vitu vinne ni lazima vitekelezwe, mosi, mbinu wazi na mamlaka maalum ya polisi, pili, utaratibu sanifu kuhusu ujenzi wa taasisi, tatu, mshikamano fanisi na nne ujuzi na utaalamu wa vipengele vinavyohitajila kujenga taasisi fanisi ya polisi.

Kuhusiana na Ebola Kamishna Hinds amesema

SAUTI YA HINDS

"Ningependa pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia kwa baraza na nchi zinazochangia polisi kwa msaada tuliopokea wakati wa janga la Ebola. Kujitolea na kujituma kwa maafisa wenu wa polisi kumekuwa na kutabakia kuwa muhimu katika kudumisha amani, utulivu na usalama katika wakati wa changamoto isiyokuwa ya kawaida.