Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania inanufaika vilivyo kwa mkutano wa lishe :Dk Rashid

Tanzania inanufaika vilivyo kwa mkutano wa lishe :Dk Rashid

Mkutano kuhusu lishe ukiendelea mjini Roma Italia, wawakilishi mbalimbali wa nchi wameelezea namna unavyonufaisha nchi zao katika mustakabli mzima wa chakula na lishe.

Miongoni mwao ni waziri wa afya wa Tanzania Dk Seif Rashid ambaye katika mahojiano maalum na Leda Letra wa radioya Umoja wa Mataifa amesema hii ni fursa kwa nchi yake kujifunza namna bora ya uhifadhi na uzalishaji bora na endelevu wa chakula. Kadhalika Dk Rashid amesema Tanzania inatekeleza mikakati ya kukuza lishe bora na kuiainisha.

Kwanza anaanza kueleza namna nchi inavyonufaika kupitia mkutano huo.