Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya haki za binadamu yajibu tuhuma nyingi za uvunjwaji wa haki za binadamu Eritrea

Tume ya haki za binadamu yajibu tuhuma nyingi za uvunjwaji wa haki za binadamu Eritrea

 Wachunguzi wamenza utafiti nchini Eritrea ambapo baraza la haki za binadamu limelaani kile ilichokiita kuenea kwa mifumo ya uvunjaji wa haki za msingi za binadamu.

Tuhuma hizo ni pamoja na mauaji yasiyo halali ,utesaji, ukamatwaji holela,uwekwaji kizuizini na kulazimishwa kujiunga na jeshi. Kwa mujibu wa mkuu wa uchunguzi huo Mike Smith maelfu ya vijana na wazee wamekimbia nchi.

(SAUTI MIKE)

 "Watu hawa wanaondoka nchini mwao kwa sababu, na watu kawaida hawajiingizi katika hali ya hatari na hali ya kiwewe, ambayo watu wengi  wanafanya, na hatari ya kutumikishwa na wafanyabiashara haramu na kadhalika na kusafiri katika maeneo hatari kwa mashua katika mediterenia bila ya sababu, na hii ndiyo sababu kwanini tutafuatilia kwa ukaribu."

 Makamishina watatu wa Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza mjini Geneva alhamisi hii waliwaita mashahidi kuja mbele na taarifa zinazoweza kusaidia katika uchunguzi wao. Bwana Smith aliita orodha hiyo ya tuhuma za ukiukwaji kuwani ndefu na endelevu lakini akasema kuwa mamlaka ya Eritrea haijaitikia wito wa tume kuingia nchini humo.

Amesema ikiwa hilo litashindikana wachunguzi wanapanga kukusanya ushahidi kutoka kwa wakimbizi na watafuta hifadhi katika nchi jirani ikiwamo Ethiopia na Sudan.

Ikiwa uchunguzi utafanikiwa  itakuwa ni hatua kubwa kwa raia hususanipale ambapo serikali itachukua hatua kuwasaidia. Kamisheni ya uchunguzi inapaswa kutoa matokeo ya mapendekezo yake.