Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwepo wa Papa Francis kwenye ICN2 umenigusa: Makene

Pope Francis (Kulia) akiwa na Mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano Da Silva kwenye mkutano wa ICN2 mjini Roma, Italia. (Picha:FAO Facebook)

Uwepo wa Papa Francis kwenye ICN2 umenigusa: Makene

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu lishe unaendelea huko huko Roma, Italia ambapo viongozi mbali mbali wanahutubia wakipigia chepuo haki ya chakula na lishe bora.

Miongoni mwao ni kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis ambaye uwepo wake kwenye mkutano huo uliibua hisia miongoni mwa washirika wa mkutano na mashuhuda.

Mmoja wao ni Boniphace Makene, Afisa habari kutoka ofis ya makamu wa Rais nchini Tanzania ambaye hakuficha hisia zake alipohojiwa na Stéphanie Coutrix wa Radio ya Umoja wa Mataifa mjini Roma.