Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tija pekee kwenye kilimo haitoshi tuweke na viwanda karibu:Kutesa

Nchini Rwanda, moja ya mifano ya viwanda vya kuboresha thamani kwenye mazao. (Picha:UNIDO)

Tija pekee kwenye kilimo haitoshi tuweke na viwanda karibu:Kutesa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amesema uwekezaji kwenye sekta ya kilimo uwe zaidi ya kuongeza tija kwenye sekta hiyo ambayo bado muhimu kwa maendeleo ya Afrika na hivyo kuinua kipato na kuweka uhakika wa chakula.

Amesema hayo kupitia msaidizi wake Balozi Arthur Kafeero wakati wa tukio lililofanyika kwenye Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya maendeleo ya viwanda barani Afrika yenye maudhui,  Maendeleo endelevu jumuishi-Viwanda vya bidhaa za kilimo barani Afrika kwa uhakika wa chakula.

Kutesa amesema uzalishaji wa mazao umeongezeka lakini bado kuna mkwamo katika kuongeza thamani ya mazao hayo pale yanapolimwa na kiasi kikubwa hupotea wakati yanaposafirishwa na hata kiwango cha utumiaji wa zao husika unakuwa na ukomo. Hivyo akatoa pendekezo.

(Sauti ya Kafeero)

“Jitihada kubwa na uwekezaji ni lazima zijikite kwenye uanzishaji wa mifumo ya kubadili mazao ya kilimo baada ya kuvunwa. Kasi kubwa ya kuendeleza viwanda vya kuboresha mazao ya kilimo haikwepeki. Na kadri mabadiliko haya yanapofanyika ni muhimu watunga sera wakazingatia uendelezaji wa sekta ya kilimo ambayo inaajiri asilimia 65 ya wakazi wa Afrika na inachangia theluthi moja ya pato la ndani la bara hilo.”