Wanawake wabunge Tanzania ni wachapakazi: Anne Makinda

Picha: Joseph Msami

Wanawake wabunge Tanzania ni wachapakazi: Anne Makinda

Wakati kikao cha maandalizi ya mkutano wa maspika wa bunge kikimalizika mjini New York, spika wa bunge kutoka Tanzania Anne Makinda amesema wabunge wanawake nchini humo wamefanya kazi kubwa katika kuleta mabadiliko juu ya mtizamo wa watu kuhusu wanawake kwenye jamii.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa spika Makinda ambaye kwa sasa ni rais wa bunge la nchi za kusini mwa Afrika SADC amefafanua wajibu wa bunge hilo. Kwanza anaanza kwa kueleza kile kilichojadiliwa na kikao hicho cha maandalizi cha mkutano wa maspika kwa mwaka 2015.

(SAUTI MAHOJIANO)