Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubunifu utumike kuboresha haki za watoto:UNICEF

Wanafunzi wakifurahia kwani hapa wana uhakika wa haki ya msingi ya kuendelezwa kutekelezeka. (Picha:UNICEF)

Ubunifu utumike kuboresha haki za watoto:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa ripoti ya hali ya watoto duniani kwa mwaka huu wa 2014 inayotaka hatua zichukuliwe kubuni mambo yatakayoboresha haki za mtoto. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Ripoti imetolea mfano Nigeria ambako wasichana wanne wamebuni jenereta inayotumia mkojo kuzalisha umeme na hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa umeme ikiwemo shuleni.

Huko Bangladesh nako ubunifu wa shule zinazoelea umewezesha watoto kwenye maeneo yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara kuhudhuria shule mwaka mzima tofauti na awali.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Anthony Lake amesema ni lazima dunia kuwa na ubunifu zaidi ili ubunifu uweze kuwa na maslahi zaidi akisema katika zama za sasa za utandawazi suluhisho katika eneo moja linaweza kuwa na manufaa kwa jamii nyingine.