Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu ni kigezo muhimu cha maendeleo kwani ndio utajiri halisi wa nchi: Chauwdry

Nembo ya IPU @IPU

Watu ni kigezo muhimu cha maendeleo kwani ndio utajiri halisi wa nchi: Chauwdry

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema wabunge ni muhimu kwa kila sehemu ya ajenda ya kuendeleza amani, maendeleo na haki za binadamu akisema wao ni daraja baina ya wananchi na jamii, taifa na mataifa.

Ametoa kauli hiyo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York wakati wa mkutano wa Umoja wa mabunge duniani, IPU wenye lengo la kuhakikisha malengo endelevu yanajikita kwenye maslahi ya wananchi.

Ban amesema kufikia maendeleo endelevu kutategemea hatua katika ngazi ya kitaifa ya kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kimataifa.

Kwa mantiki hiyo amesema bunge litakuwa na jukumu kuu katika kutafsiri na kurekebisha ajenda ya kimataifa katika mabadiliko ya kweli mashinani mathalan kupitia sheria, mageuzi ya fedha, ushiriki imara wa raia, usimamizi madhubuti na uwajibikaji.

Suala hilo la kupatiwa wananchi kipaumbele kwenye mchakato wa ajenda wa maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 likapigiwa chepuo na Rais wa IPU Saber Hossain Chowdhury.

(SAUTI CHAUDRY)

Ni lazima kutazama wananchi kama utajiri wa kweli wa mataifa, na kwa hiyo watu wawe wanufaika na waendeshaji halisi wa mchakato huu.”