Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna sababu lukuki za kupigia chapuo siku ya choo duniani: Eliasson

UN Photo/Amanda Voisard
Picha:

Kuna sababu lukuki za kupigia chapuo siku ya choo duniani: Eliasson

Kuna sababu za kiuchumi, na kijamii kujadili umuhimu wa usafi na maji katika kuadhimisha siku ya choo duniani amesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Bwana Eliasson amesema ikiwa maji na usafi utazingatiwa huongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa jamii husika. Naibu Katibu Mkuu akaenda mbali zaidi na kusisitiza.

(SAUTI ELIASSON)

"Ni suala la haki za binadamu. Haki ya maendeleo ni haki ya maji na usafi ambayo imeanzishwa na baraza la haki za binadamu na baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Kwangu pia ni suala la utu."

Kwa upande wake balozi wa Singapore katika Umoja wa Mataifa Karen Tan amesema nchi yake inaendeela kupigia kampeni uwepo wa vyoo na usafi kwa kuwa bado dunia inahitaji kuelimishwa zaidi kuhusu suala hilo akisema kuwa bado watu wangu hawataki kuzungumzia masuala ya choo hadharani.

Akiongea katika mkutano huo mkuu wa shirika la kimatifa la hali ya hewa WMO, Michel Jarraud amesema ukosefu wa huduma muhimu za kujisafi na maji ni moja ya chanzo kikuu cha mlipuko wa homa ya Ebola inayoendelea Afrika Magharibi.