Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali nyingi duniani zimeanza kupiga hatua –ILO

Picha: ILO

Serikali nyingi duniani zimeanza kupiga hatua –ILO

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani ILO Emmanuel Julien amesifu namna maneneo mbalimbali duniani yalivyopiga hatua kuwa kuweka sera na kutekeleza mikakati ambayo imefanikisha masuala ya kazi na uzalishaji wa ajira.

Julien ambaye anahusika zaidi na kitendo cha ujasilimali ndani ya ILO amesema kuwa kumeendelea kushuhudiwa mabadiliko makubwa ya kutia moyo ikiwamo kwa serikali nyingi kuanzisha utaratibu ambao unahimiza kufuata kanuni stahiki sehemu za kazi.