Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki watumika kuondoa kiwewe miongoni mwa wakimbizi

Fabian Kamasa na gitaa lake atumialo kwenye harakati zake za kuwanasua wakimbizi kutoka kwenye kiwewe. (Picha: Kwa hisani ya John Kibego)

Muziki watumika kuondoa kiwewe miongoni mwa wakimbizi

Ghasia na mizozo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imesababisha baadhi ya wananchi kukimbilia nchi jirani na miongoni mwa nchi hizo ni Uganda. Wakimbizi hao wakati madhila hayo yakiendelea na hata wakiwa njiani wakisaka hifadhi hushuhudia au hata hukumbwa na visanga vingi ikiwemo vipigo, mateso na hata ubakaji ambavyo husababisha matatizo kama vile kiwewe. Baadhi yao wamesaka hifadhi kwenye kambi ya Kyangwali nchini Uganda ambako stadi mbali mbali hutumika kuwaondoa kwenye mazingira ya kiwewe. Je ni mbinu zipi? Ungana basi na John Kibego wa Radio washirika Spice FM kutoka Uganda.