Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vurugu zakatisha matumaini wakazi wa Sahel: Piper

Robert Piper akizungumza na wakulima maeneo ya Timbuktu @OCHAROWCA

Vurugu zakatisha matumaini wakazi wa Sahel: Piper

Mratibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Sahel, Robert Piper amesema kwa mara nyingine tena eneo la Ukanda wa Sahel linakabiliwa na ukosefu wa usalama, huku matumaini ya kuboreka kwa hali ya mamilioni ya watu wanaoishi katika mazingria magumu yakididimia. Taarifa kamili na Abdullahi Halakhe.

(Taarifa ya Abdullahi)

Bwana Piper katika tathmini yake amesema wadau wa kikanda wanahitaji kukabiliana na chamgamoto za kiusalama au watakabiliwa na hatari zaidi mwakani.

Amesema watu wa Sahel wameathiriwa na ukame na njaa, lakini vurugu za hivi karibuni zimeongeza zaidi idadi ya wakimbizi akitolea mfano Nigeria ambapo watu Milioni Moja na Nusu wamekimbia makwao kutokana na vitendo vya kundi la kigaidi la Boko Haram.

(SAUTI PIPER)

Kilichobadilika ni ukubwa wa tatizo la Boko Haram! Limesababisha mateso juu ya mateso, lingaongeza idadi ya wakimbizi. Katika kipindi cha miezi minne idadi imeongezeka kati ya 600 na Elfu Moja hadi aidi ya watu Milioni Moja na Nusu, na hii ni kwa mujibu wa mamlaka ya Nigeria”