WHO yatiwa moyo kutosambaa kwa binadamu kwa kirusi kipya cha ndege H5N8

18 Novemba 2014

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema  mlipuko wa hiivi karibuni wa homa ya mafua ya ndege haujaambukiza binadamu na kwamba unaweza kutibiwa kwa dawa zilizopo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva daktari wa WHO Elizabeth Mumford amesema kirusi aina ya H5N8 hakitabiriki na kwamba kinafanana na kile kiitwacho H5N1 ambacho kilisababisha magonjwa kwa binadamu na wanyama barani Asia na nchini Msri, Afrika.

 Amesema kuwa wakati bado hakuna ufahamu wa kutosha kuhusu kirusi, utafiti wa awali unaonyesha kuwa kinalenga ndege kuliko wanadamu.

 Kadhalika amesema kirusi hicho kinaweza kutibika kwa kutumia dawa ya kwanza aina ya Tamiflu

 (SAUTI DK MUMFORD)

 “Kama tunavyofahamu sote virusi vya ndege havitabiriki nan i vigumu kusema kirusi kipya kitanya nini. Kile ninachoweza kuwaeleza ni kwamba kumekuwa na visa vya binadmau ambavyo vimeripotiwa licha ya kwamba kirusi kinazunguka kwa kuku kwa muda mrefu huko Asia. Tuna tatizo la utambuzi ikiwa kinasababisha magonjwa makali kwa binadamu hatuwezi kufahamu watu wangapi wameathiriwa lakini tunafahamu kuwa kuna ufuatiliaji kwa nchi hizi tatu. Kwahiyo ukweli kwamba hatuoni idadi kubwa ya watu ya visa vya watu hili linatia moyo.”

Kirusi hicho kinachotajwa kusambazwa kupitia ndege wanaohama kutoka Asia kilionekana kwa mara ya kwanza Korea, Japan, na China na sasa kimeripotiwa katiak nchi za Ulaya ambazo ni Uholanzi na Ujerumani

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter