Hali ya sasa kuhusu mzozo wa Ukraine si endelevu -Ban

15 Novemba 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa ulimwengu umegawanyika kuhusu mzozo wa Ukraine kama nyakati za vita baridi, na kuonya kuwa hali hiyo ya sasa haiwezi kuwa endelevu kwa ajili ya amani ya dunia nzima na uchumi.

Katibu Mkuu amesema hayo wakati mkutano wa siku mbili wa nchi 20 tajiri zaidi duniani na zile zinazoibuka kiuchumi, yaani G20, ambao unafanyika mjini Brisbane, Australia.

Bwana Ban amewasihi wanachama wa G20 kujadili suala la Ukraine pembezoni mwa mkutano huo.

Ban pia amezungumzia masuala kadhaa muhimu, likiwemo tatizo la mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud