Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwajibishwaji haukwepeki DPRK: Mtaalamu

Makao Makuu ya UM(picha ya UM)

Uwajibishwaji haukwepeki DPRK: Mtaalamu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya watu wa Korea (DPRK) Marzuki Darusman amesema suala la uwajibishwaji kwa wanaotenda uhalifu kinyume na binadmau nchini humo linasalia ajenda muhimu

Akiongea baada ya kuhitimisha ziara yake mjini Seoul, Bwana Darusman amesema maoni hayo yanakuja muda mfupi kabla ya kamati ya tatu ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa kupigia kura azimio la kuifikisha DPRK katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kwa ukatili dhidi ya binadamu.

Wiki mbili zilizopita mtaalamu huyo kwa mara ya kwanza alikutana na wawakilishi wa maafisa wa ngazi ya juu wa DPRK ambao walimualika katika ziara hiyo kwa masharti kuwa viongozi wote wa Korea ya Kaskazini waliojumuishwa katika orodha ya kuwajibishwa na kufikishwa ICC waondolewe

Bwana Darusman amesema anapaswa kualikwa DPRK bila masharti yoyote na kutoheshimiwa kwa azimio huku akisisitiza kuwa kuanzia sasa ni vyema kufikiri kuanza mazingira kwa ajili ya mchakato wa uwajibishwaji.

Taarifa zitakazokusanywa na mtaalamu huyo  zitajumuishwa katika ripoti yake baraza la haki za binadamu mwezi March mwaka 2015.