Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujuzi wa wahudumu na tiba sahihi vyapunguza Numonia Tanzania:UNICEF

Mtoto mchanga amezaliwa, hapa ni hospitali ya mkoa wa Mbeya, Tanzania. (Picha: © UNICEF/UNI161878/Holt)

Ujuzi wa wahudumu na tiba sahihi vyapunguza Numonia Tanzania:UNICEF

Takwimu mpya za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF zinaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto wachanga kutokana na ugonjwa wa Numonia au vichomi. Mathalani ikilinganishwa na mwaka 2000 kiwango cha vifo sasa kimeshuka kwa asilimia 44 lakini UNICEF inasema hatua lazima ziendelee kuchukuliwa kwani Numonia inaua watoto wengi kuliko hata Ukimwi. Je nchini Tanzania hali ikoje? Assumpta Massoi wa Idhaa amezungumza na Dkt. Thomas Lyimo mtaalamu wa afya katika Idara ya Afya na Lishe ya UNICEF, Tanzania na  hapa anaanza kwa kuelezea hali ya Numonia nchini  humo.