Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zatakiwa zijikite upya katika elimu- lasema kongamano la Aichi-Nagoya

Elimu nchini India.(Picha ya UM/C Srinivasan)

Serikali zatakiwa zijikite upya katika elimu- lasema kongamano la Aichi-Nagoya

Kongamano la kimataifa kuhusu elimu kwa ajili ya maendeleo endelevu (ESD) limehitimishwa leo mjini Aichi-Nagoya, Japan, kwa azimio linalotaka hatua zichukuliwe haraka kujumuisha elimu kwa maendeleo endelevu katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Azimio la Aichi-Nagoya linatoa wito kwa nchi zote kutekeleza mkakati wa kimataifa wa kuchukua hatua kuhusu elimu kwa maendeleo endelevu (GAP) ili kuendeleza ajenda ya mkakati huo wa ESD.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja washiriki zaidi ya 1,000, chini ya kauli mbiu: “Kusoma leo kwa mustakhbali endelevu.” Mkakati wa GAP unatarajiwa kujikita katika masuala ya uungaji mkono kisera, kumulika taasisi za elimu, walimu, vijana na jamii za mashinani.