Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uingereza yachangia mfuko wa kuisadia Sudan

UN Photo/Albert Gonzalez Farran
Nchini Sudan.

Uingereza yachangia mfuko wa kuisadia Sudan

Serikali ya Uingereza imetoa kiasi cha Dola za Marekani milioni 11.3 kwa ajili ya kupiga jeki mfuko wa pamoja na kuikwamua Sudan. Kiasi hicho cha fedha kinafuatia kiasi kingine cha Dola milioni 16.4 kilishotolewa na serikali hiyo hivi karibuni.

Hali ya ustawi wa kibinadamu nchini Sudan inaelezwa kuzorota kwa kiasi kikubwa hivyo kuendelea kutolewa kwa fedha hizo kutatoa mwanga wa matumaini kwa wananchi wa eneo hilo.