Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yachunguza tuhuma za kubakwa kwa mamia ya wanawake Darfur

Walinda amani walioko Darfur wakiwa katika moja ya doria zao. (Picha:Albert González Farran, UNAMID)

UNAMID yachunguza tuhuma za kubakwa kwa mamia ya wanawake Darfur

Ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni Darfur (UNAMID) umeeleza kusikitishwa kwake na taarifa za hivi karibuni katika vyomba vya habari kuhusu ubakaji wa halaiki uliohusisha wanawake na wasichana  200 kaskazini mwa Darfur na kuelezea nia ya kufanya uchunguzi kupata ukweli wa ripoti hizo.

Taarifa ya UNAMID inasema katika kutekeleza hilo imetuma doria ya uhakiki November nne mwaka huu licha ya kwamba doria hiyo ilikumbana na kikwazo nje kidogo ya mji  cha kutoka kwa cha jeshi la Sudan. Kwa mujibu wa UNAMID licha ya juhudi za majadiliano doria hiyo haikufanikiwa kupenya kuingia Tabit eneo kunakodaiwa kufanyiak ubakaji huo.

Ujumbe huo unazitaka mamlaka nchini Sudan kuwezesha ufikiwaji wa wa maeneo kwa ajili ya uchunguzi hususani eneo ambalo tuhuma za matukio yaliyoathiri raia zimeripotiwa kulingana na mkataba unaowaruhusu walinda amani kutekeleza majukumu yao bila vizuizi katika mazingira kama hayo (SOFA).

Ikiwa ni sehemu ya uchunguzi afisa wa haki za binadmau wa UNAMID amekutana na mwendesha mashtaka mkuu wa kaskazini mwa Darfur ambaye amesema kuwa hakuna malalamiko yoyote yaliyopokelewa kuhusu ubakaji kutoka Tabit.