Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Asia zahimizwa kufunguka zaidi kiuchumi

Picha: UNCTAD

Nchi za Asia zahimizwa kufunguka zaidi kiuchumi

Nchi zilizoko katika ukanda wa Asia ambazo hazijapitiwa na bahari zimehimizwa kufungua milango ya kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba zinapanua fursa zaidi za kimaendeleo kwa ajili ya kukuza uchumi.

Wito huo umetolewa na Kamishina ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya maendeleo na kijamii kwa Asia na Pacific (ESCAP).

Kamishina hiyo imesema kuwa nchi hizo zinapaswa kubainisha fursa mpya ambazo zitasaidia kusukuma mbele shughuli za kimaendeleo.

Pia zimetakiwa kupitia upya sera zake kwa ajili ya kwenda sambamba na ushindani wa soko unaoendelea kujitokeza sasa.