Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walengwa 700 huko Gaza wapata vifaa vya Ujenzi : Serry

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mashariki ya Kati, Robert Serry wakati wa kikao cha Baraza la Usalama.Picha/UM/Loey Felipe

Walengwa 700 huko Gaza wapata vifaa vya Ujenzi : Serry

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani Mashariki ya Kati, Robert Serry amethibitisha kwamba utaratibu wa ujenzi wa muda wa Gaza umeanza kazi huku upatikanaji wa vifaa vya ujenzi ukiwa unapatiwa kipaumbele.

Katika taarifa, Serry amesema, kufikia Jumatatu jioni, walengwa 700 waliweza kununua vifaa muhimu vya ujenzi ili kuanza ukarabati wa nyumba zao baada ya mashambulio makubwa ya hivi karibuni huko Gaza.

Amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kuhamasisha kila jitihada ili kuhakikisha mfumo huo unawanufaisha Wapalestina Gaza na katika kiwango cha kushughulikia mahitaji yao makubwa ya ujenzi Gaza.

Halikadhalika, Serry amesema, utaratibu huo unaongozwa na Serikali ya Kitaifa ya Makubaliano ya Palestina, ikishhirikiana na sekta ya kibinafsi Gaza