Vijana wasipokuwa na cha kufanya wako hatarini kutumbukia katika uhalifu:Ban

4 Novemba 2014

Jukwaa la ubia wa kuchagiza viwanda vyenye kuleta maendeleo endelevu limefanyika huko Vienna, Austria ambapo Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema vijana licha ya kuwa na uwezo, stadi, nguvu na mawazo mazuri bado wengi wao hawana ajira.

Amesema duniani kote vijana Milioni 75 hawana ajira jambo ambalo linaweza kusababisha wajitumbukize katika Imani zenye misimamo mikali, ugaidi na uhalifu.

Ban amewaeleza washiriki wa jukwaa hilo lililoandaliwa na shirika la maendeleo ya viwanda la Umoja wa Mataifa, UNIDO kuwa vijana wana uwezo wa kuchagiza kuanzisha viwanda endelevu vinavyoweza kutoa fursa za ajira.

Kwa mantiki hiyo amesema ni vyema jamii kuwa sekta ya uchumi inayojumuisha makundi yote ili hatimaye kuwa na hakikisho la usalama na amani ya kudumu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter