Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 173 zahitajika kwa msimu wa baridi kali Iraq-OCHA

Mvulana huyu asimama kandoni mwa msaada uliowasilishwa na WFPA huko Mala jimbo la Erbil Governorate, kaskazini mwa Iraq. (Picha ya OCHA/Iason Athanasiadis)

Dola milioni 173 zahitajika kwa msimu wa baridi kali Iraq-OCHA

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola milioni 173.1 ili kusaidia kukidhi mahitaji ya watu wapatao milioni 1.2 nchini Iraq, ambao wanahitaji usaidizi katika msimu wa baridi kali unaoanza. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini humo, Jacqueline Badcock, amesema kuwa rasilmali zaidi zinahitajika kwa dharura kwani watu waliopoteza makazi yao tayari wanakabiliana na mvua nzito, upepo, kimbunga na hali ya baridi.

Tangu Januari mwaka 2014, watu milioni 1.9 wamelazimika kuhama makwao nchini Iraq, wengi wao wakikimbia bila chochote, ila nguo walizovaa tu. Takriban asilimia 50 kati yao wamekimbilia maeneo ya milimani katika jimbo la Kurdistan, ambako kuna baridi kali zaidi msimu wa baridi, wakati mwingine ikifikia nyuzi sifuri.