Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wa UM wajeruhiwa CAR

Stephane Dujarric,Picha ya UM

Walinda amani wa UM wajeruhiwa CAR

Wanajeshi tisa wa kikosi cha kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa walijeruhiwa baada ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA kufanya operesheni ya usalama kwa kushirikiana na kikosi cha Kitaifa cha Sangaris katika wilaya mbili mjini Bangui siku ya Ijumaa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kikosi cha MINUSCA kiliwakamata watu watano pamoja na silaha na risasi wakati wa operesheni hiyo.

Japo kuna changamoto, Dujarric ameelezea ujumbe wa MINUSCA umekariri azma yake ya kutekeleza wajibu wake licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu.