Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubadili vipaumbele si kupunguza majukumu yetu Sudan kusini:UNMISS

Ellen Margrethe Løj.(Picha ya UM)

Kubadili vipaumbele si kupunguza majukumu yetu Sudan kusini:UNMISS

Kubadilika kwa vipaumbele vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS hakumaanishi kupunguza ushiriki wake kwenye azma ya ulinzi wa amani.

Hayo yamesemwa na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Ellen Margrethe Løj wakati akizungumza mwishoni mwa mkutano wa nne wa magavana kwenye mji mkuu Juba.

Ametoa ufafanuzi huo kufuatia uamuzi wa baraza kuu wa kuongeza muda wa UNMISS hadi tarehe 30 mwezi huu ikiweka kipaumbele katika ulinzi wa raia, ufuatiliaji wa haki za binadamu na usaidizi wa misaada ya kibinadamu.

(Sauti ya Løj)

"UNMISS pia inaangalia jinsi ya kusaidia taasisi za kitaifa katika kuchagiza harakati za kushughulikia mizozo pamoja na kuleta maridhiano baina ya jamii kama tunavyofanya kwenye jimbo la Lake. Mtazamo wangu wa wazi ni kwamba jamii ya kimataifa bado ina matumaini kuwa suluhu la kisiasa litapatikana karibuni.”

Halikadhalika, Bi. Løj amesisitiza umuhimu wa kusaka suluhu ya mzozo wa Sudan Kusini kwa njia ya Amani akisema hakuna mbadala wa kuacha mapigano.