Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaalani uharibifu vituo vya kitamaduni Iraq

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokova nchini Iraq.(Picha ya UNAMI)

UNESCO yaalani uharibifu vituo vya kitamaduni Iraq

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokova ameunga mkono serikali ya Iraq kwenye juhudi zake za kupambana na uharibifu wa vituo vya utamaduni nchini humo unaofanywa na kundi la ISIS.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano uliwaleta pamoja watu wa makundi mbalimabli Bokova alilaani vitendo vya kuendelea kuwatesa na kuwaangamiza watu wasio na hatia akisema kuwa hali kama hiyo inapaswa kukomeshwa.

Alisema  kuwa Iraq na watu wake wanahifadhi moja ya mali zenye thamani kubwa za utamaduni ambazo ni muhimu kwa ulimwengu hivyo lazima zilindwe tena kuhifadhiwa kwa hali yoyote.

Amesema Iraq ina maelfu ya mahekalu, majengo, sehemu za kale na haitakubalika kuziharibu