Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Martin Kobler awataka vijana kulijenga taifa la DRC

Vijana wa DRC wakati wa maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa.(Picha ya MONUSCO/Myriam Asmani)

Martin Kobler awataka vijana kulijenga taifa la DRC

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo  Martin Kobler amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na vijana kulijenga taifa lao.Akizungumza kwenye maadhimisho ya tatu ya siku ya vijana wa Afrika, Kobler hata hivyo aliwataka vijana kuendelea kujituma zaidi ili kusuka mbele ustawi wa taifa lao.

 Alisenma kuwa raia wa Congo wanaume kwa wanawake wanalojukumu la kuboresha mstakabali wa taifa lao kwa kuhakikisha linaenzi la kuendeleza amani na utulivu.

Mkuu huyo wa MONUSCO alisema kuwa wananchi hao wanalo jukumu la kushiriki kikamilifu kwenye masuala yahusuyo siasa, uchumi na yale ya kiutamaduni akisema kuwa kwa kufanya hivyo watasaidia ustawi wa taifa la Kongo nzima.