Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waandishi ni kiungo muhimu katika jamii, walindwe: Kutesa

UN Photo/Devra Berkowitz
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Sam Kutesa,(

Waandishi ni kiungo muhimu katika jamii, walindwe: Kutesa

Dunia inapoadhimisha kwa mara ya kwanza siku ya kimataifa ya kukomesha ukwepaji sheria dhidi ya uhalifu kwa waandishi wa habari November mbili , rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amesema wanahabari wana umuhimu mkubwa katika ujenzi wa jamii huru na wazi ambayo wanajamii huamua kulingana na kupata taarifa.

Katika taarifa yake iliyojikita kwenye madhimisho ya siku hiyo Kutesa amesema wanahabari huangazia hatma za jamii zilizo kwenye mizozo, watu wanosimamia haki zao za msingi, kujikamua kwenye umaskini na mazingira hatarishi

Amesema licha ya juhudi za kundi hilo, maisha yao yamekuwa hatarini akitolea mfano kuwa muongo uliopita wanahabari 700 walipoteza maisha yao huku wengi wao wakiwa wahanga wa vitisho, vifungo, unyanyasaji, utekaji nyara na mteso.

Rais wa baraza kuu amezitaka nchi wanachama kuchukua hatua muhimu katika kuweka mazunguira mazuri ya kazi kwa waandishi wa habari pamoja na kuhakikisha wanaendesha mashtaka ya uhalifu dhidi yao.

Siku ya kimataifa ya kukomesha ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari ilipitishwa kupitia azimio la baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana likitoa majukumu kwa UNESCO kutekeleza siku hiyo inayopigia chapuo haki ya jamii ya kupata taarifa.