Burkina Faso: Ban afahamu kuhusu kujiuzulu kwa Rais Compaoré

31 Oktoba 2014

Wakati mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Afrika Magharibi Mohammed Ibn Chambas akiwa amewasili Burkina Faso kusaka suluhu la mzozo unaoendelea nchini humo, Ban Ki-Moon ametambua hatua ya karibuni zaidi ya kujiuzulu kwa Rais wa nchi hiyo Blaise Compaoré.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema pamoja na kutambua hali hiyo, Katibu Mkuu anafuatilia kwa wasiwasi mkubwa uzorotaji wa amani nchini humo.

Bwana Chambas akiwa ameambatana na wajumbe kutoka jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS na Muungano wa Afrika, anatarajiwa kukutana na wadau wa siasa, viongozi wa kijadi na kidini.

Vyombo vya habari vimedokeza kuwa Rais Compaoré ambaye ameongeza Burkina Faso kwa miaka 27 sasa alitangaza kujiuzulu wakati huu ambapo maelfu ya waandamanaji wamekuwa wakiandamana kwenye mji mkuu Ouagadougou wakikabiliana na vikosi vya usalama .

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter