Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa kuhifadhi nyaraka za picha na sauti

Kumbukumbu za Umoja wa Mataifa.(Picha ya UM/Paulo Filgueiras)

Umuhimu wa kuhifadhi nyaraka za picha na sauti

Urithi wa picha na sauti zitokanazo na matukio mbali mbali duniani uko hatarini! Hii imesababishwa na mambo mbali mbali ikiwemo: utunzaji duni, maendeleo ya kiteknolojia na uharibifu wa makusudi.Hii imesababisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuamua  kutenga siku maalum ya kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kuhifadhi kumbukumbu hizo. Kwa mantiki hiyo UNESCO inatambua Oktoba 27 kama siku ya kimataifa ya urithi wa taarifa za picha na sauti.

Kauli mbiu ya mwaka huu ambayo imeadhimishwa wiki hii ni “Kumbukumbu hatarini:Mengi yafanyike.” Katika ujumbe wake kwa siku hii mkurugenzi mkuu wa UNESCO, Irina Bokova amesema ni muhimu kuhifadhi nyaraka za picha na sauti kwa ajili ya vizazi vijavyo akiongeza kuwa urithi huo unabeba mafunzo, taarifa na ufahamu ambao ni muhimu kuhamishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hata hivyo licha ya umuhimu huo bado kumbukumbu hizo muhimu zinaendelea kupotea .Je nchi Afrika Mashariki zinatambua ni nini kuhusu umuhimu wa kumbukumbu hizi basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.