Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa IAEA kuzuru Japan kuwasilisha ripoti ya tathmini za maabara

watalaam wa IAEA wakipima maji ya bahari, karibu ya Fukushima. @IAEA/David Osborn

Wataalam wa IAEA kuzuru Japan kuwasilisha ripoti ya tathmini za maabara

Wataalam wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, wanatarajiwa kuzuru Japan kuanzia tarehe 4 hadi 7 Novemba ili kuwasilisha ripoti kuhusu kulinganisha tathmini za maji ya baharini zilizofanywa na maabara za Japan na za IAEA, na pia kutathmini vipimo vya ubora wa maabara 30, zikiwemo 12 kutoka Japan.

Wataalam hao pia watachukua sampuli mpya kutoka maji ya pwani ya karibu na mtambo wa nishati ya nguvu za Atomiki wa Fukushima Daiichi.

Wataalam hao ni, David Osborn, Mkurugenzi wa maabara za mazingiza za IAEA, Monaco na Iolanda Osvath, Mkuu wa Maabara ya vipimo vya miyale ya atomiki katika IAEA.

Kulinganisha kwa ubora wa vipimo vya maabara kunalenga kuongeza uwazi na imani katika matokeo ya ufuatiliaji wa athari za miyale ya nguvu za atomiki kwa maji ya bahari, na kuwasilisha matokeo hayo kwa umma kwa njia iliyo sahihi kisayansi na inayoweza kueleweka.