Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga la chakula lanukia Somalia: FAO

Ufugaji nchini Somalia hususan maeneo ya kusini uko mashakani kutokana na mafuriko yaliyokumba eneo hilo karibuni. (Picha:FAO)

Janga la chakula lanukia Somalia: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema linahitaji dola Milioni 49 kwa ajili ya kuokoa watu walio hatarini kukumbwa na janga la njaa nchini Somalia. Taarifa kamili na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Mkurugenzi Msaidizi wa FAO kanda ya Afrika Bukar Tijani amesema janga hilo linatokana na mazingira ya sasa kusini mwa nchi hiyo ambako baada ya msimu wa mvua usioridhisha sasa kuna mafurikio hali inayotishia usalama wa chakula.

Amesema tishio hilo linakuja wakati bado janga la njaa la mwaka 2011 liko kwenye fikra za wananchi na kwa mara nyingine tena Somalia inaweza kujikuta kwenye janga la kibinadamu.

Mathalani zaidi ya watu milioni Moja wanahitajika msaada wa dharura, ikiwa ni ongezeko kwa asilimia 20 ndani ya kipindi cha miezi Sita ilhali watu wengine Milioni Mbili wanakabiliwa na kitisho cha ukosefu wa chakula.

Tijani amesema kwa sasa wanaweza kusaidia watu 210,00 pekee lakini wanahitaji fedha walizoomba ili waweze kufikia watu 350,000 zaidi hadi nusu ya kwanza ya mwaka 2015.

Uhaba wa mvua kwa kipindi kilichohitajika mwaka huu ulisababisha kiwango cha uzalishaji wa nafaka kushuka kwa asilimia Tatu