Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera dhaifu ni shubiri kwa wakazi wa mijini: Kutesa

Mji wa Simeuleu nchini Indonesia, ambao tsunami ya mwaka 2005 uliuenganisha na maeneo mengine ambapo wananchi waliamua kutumia magogo ya mnazi kujenga daraja. (Picha:UN-HABITAT)

Sera dhaifu ni shubiri kwa wakazi wa mijini: Kutesa

Ikiwa leo ni siku ya miji duniani, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amesema ukuaji wa miji hasa katika nchi zinazoendelea badala ya kuleta ahueni umeleta madhila kutokana na sera za miji zisizo na mashiko. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa siku hii kuadhimishwa, Kutesa amesema nusu ya wakazi wa dunia wanaishi maeneo ya mijini na idadi  itaongezeka lakini kupanuka kwa miji kumekuwa shubiri kwa baadhi ya wakazi hao.

“Athari za ukosefu wa mipango na uongozi ni dhahiri kwa miji mingi duniani; mathalani ongezeko la makazi duni, uhalifu na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira.”

Kutesa akigusia ujumbe wa mwaka huu wa siku hii, Ukuaji miji wenye kunufaisha watu,  amesema ukuaji una changamoto lakini unaweza kuleta ahueni..

 “Iwapo utasimamiwa vizuri, unweza kuwa chagizo kubwa la maendeleo endelevu.”