Waandishi waachwe watekeleze wajibu wao:UNESCO

31 Oktoba 2014

Kuelekea siku ya kimataifa ya kukomesha ukwepaji sheria dhidi ya uhalifu kwa waandishi wa habari November mbili , jamii imetakiwa kuhakikisha kundi hilo linaachwa litekeleze weledi wao bila kubughudhiwa kwa kuhusishwa katika matukio segemnege.

Katika mahojiano na idhaa hii Kaimu Katibu mtendaji wa tume ya taifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNECSO nchini Tanzania Dk Moshi Kiminzi, amesema pia kuwa matukio ya kihalifu kwa wanahabari nchini humo yamepungua.

(SAUTI KIMINZI)

Siku ya kimataifa ya kukomesha ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari ilipitishwa kupitia azimio la baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana likitoa majukumu kwa UNESCO kutekeleza siku hiyo inayopigia chapuo haki ya jamii ya kupata taarifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter