Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya changamoto, utalii wa kimataifa waendelea kuimarika:UNWTO

Cape of Good Hope.Afrika Kusini(Picha ya UNWTO)

Licha ya changamoto, utalii wa kimataifa waendelea kuimarika:UNWTO

Idadi ya watalii wa kimataifa imeendelea kuongezeka duniani ambapo takwimu mpya zinaonyesha kuwa kati ya Januari na Agosti mwaka huu watalii Milioni 781 walifanya safari ugenini.Shirika la utalii duniani, UNWTO limetoa takwimu hizo likisema kiwango hicho ni nyongeza kwa asilimia Tano zaidi ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Katibu Mkuu wa wa UNWTO

amesema licha ya changamoto mbali mbali duniani, bado utalii wa kimataifa umeendelea kushika kasi.

Amesema japo ni mapema mno kutathmini athari za Ebola kwenye utalii, bado wanaamini mlipuko hautakuwa na madhara makubwa kwenye utalii.

Kiukanda, eneo la Amerika lilikuwa na idadi kubwa zaidi kwa kupata nyongeza ya watalii kwa asilimia Nane ikifuatiwa na Asia-Pasifiki.

Kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahari, idadi iliongezeka kwa asilimia Tatu