Hayati Sata akumbukwa na Baraza Kuu; Alikuwa mnyenyekevu

30 Oktoba 2014

Rais wa Zambia Michael Sata aliyefariki dunia Jumanne huko Uingereza amekumbukwa leo ndani ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambapo Rais wa baraza hilo Sam Kutesa alizungumza kabla ya kuanza kwa kikao.

(Sauti ya Kutesa)

“Kabla hatujaendelea na ajenda yetu, ni kwa majonzi makubwa natoa rambambira kwa hayati Rais wa Jamhuri ya Zambia Michael Chilufya Sata ambaye amefariki dunia Jumanne tarehe 28 mwaka 2014. Kwa niaba ya baraza kuu namuomba Mwakilishi wa Zambia awasilishe rambirambi zetu kwa serikali na wananchi wa Zambia na wka familia ya Hayati Michael Chilufya Sata.”

Kutesa amesema alifahamiana na hayati Sata kwa kipindi kirefu na alikuwa mtu aliyezingatia maadili.

Wengine waliotoa rambirambi zao kwa Rais huyo wa Tano wa Zambia ni mwakilihi wa kudumu wa nchi hiyo kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Mwaba Kasese-Bota

(Sauti ya Balozi Kasese-Bota)

Rais Sata alifahamika vyema kwa umakini na uwazi wake. Halikadhalika alikuwa mcheshi, mtoaji na alionyesha kiwango kikubwa cha urafiki na unyenyekevu, tabia ambayo ni aghalabu kupatikana kwa watu wenye madaraka.”

Hayati Sata aliyezaliwa mwaka 1937 aliingia madarakani mwezi Septemba mwaka 2011 baada ya kushinda uchaguzi mkuu.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter